UKAGUZI WA SAJILI

Patrick lepakiyo

Kura ya mchujo umeweza kukamilika kote nchini sasa, na wananchi  wanategea kushiriki katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika agosti nane.

IBC

Ni dhahiri kuwa vurugu na mvutano ya hapa na pale imeweza kushuhudiwa katika teuzi hizo za vyama huku viza vya wizi wa kura vikiwa vya kutamkwa kila wakati.

Kabla ya uchaguzi mkuu ukaguzi wa sajili ya wapiga kura hufanywa ili kuhakikisha kuwa kila mkenya ambaye amesajiliwa kama mpiga kuru yuko katika sajili hiyo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Wafula chebukati amesema kuwa zoezi la ukaguzi wa sajili mpya ya wapiga kura linaanza rasmi leo na kuendelea hadi tarehe tisa mwezi juni.

Chebukati vile vile amewarai wakenya kuzuru vituo walivyojisajili kuthibitisha usajili wao na pia kujifahimisha teknolojia mpya itakayotumika wakati wa uchaguzi.

Kuthibitisha iwapo umesajiliwa kama mpiga kura itaondoa lalama za baada ya uchaguzi mkuu ujao kwa sababu kila mwananchi atarathika na matokeo ya uchaguzi huo kwani viza vya wizi wa kura vitapungua kila mwananchi akihakikisha kuwa amesajiliwa kama mpiga kura.

Kujifahamisha na teknolojia mpya itakayotumika wakati wa uchaguzi wa agosti ni muhimu kwani itakuwa rahisi kwa mpiga kura kutumia na pia hautadananywa kupigia kura mgombea ambaye hujapanga kumchagua kama kiongozi wako.

Kumbuka kura yako ni kauli yako

Advertisements

MCHUJO BARIDI

BY PATRICK LEPAKIO

Kura za mchujo zimeibuwa tumbo joto kwa baadhi ya maeneo nchini huku wagombea wa viti mbalimbali wakisemekana kuhusika na wizi wa kura.

Kumekuwa na visa vya vurugu vinavyotakana na kura hizo za mchujo huku ikisemekana kuwa na wizi ama wagombea wengine kukataa kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Baadhi ya kaunti kama vile kaunti ya busia bado watarudia kura ya mchujo hasa ile ya kiti cha ugavana ambapo ilihusisha Gavana wa sasa Sos Peter Ojamoung’ na mbunge wa funyula daktari Paul otuoma,  kuhusiana na utata unaozingira uteuzi huo wa wiki iliopita ambapo ojaamong alitangazwa mshindi huku otuoma akipinga matokeo.

Hii imepelekea  baraza la wazee kaunti ya busia kutaka bodi ya uchaguzi ya chama cha ODM kumkabidhi Otuoma Cheti cha kuwania ugavana katika kaunti hiyo.

otuma

Wazee hao wamesema otuoma alishinda kura ya mchujo kwa njia ya haki wakitishia kuongoza wakaazi wa busia kugura chama cha ODM iwapo chama hicho kitamnyima otuoma cheti cha ushindi.

 

Katika kaunti ya Uasin Gishu pia kumekuwa na kutoelewana huku ikisemekana mwaniaji wa kiti cha mbunge kupitia chama cha jubilee Mishna Kiprop amelazwa katika hosipitali ya Medihill mjini Eldoret kutokana na kichapo alichopokea kutoka kwa wafuasi wa mshindani wake Allan Kosgei.

MISHNA

 

 

DINI YA ROHO MAFUTA

NA PATRICK LEPAKIO

 

POKOT

Kanisa la new jerusalem- salama dini ya roho mafuta pole ya Afrika inayopatikana  kapenguria kaunti ya pokot magharibi.

Kanisa hili linaongozwa na rostin aburan ambaye ni karani mkuu katika kanisa hilo.

Kanisa hili lina mambo ambayo si ya kaiwada ama inatofautiana na makanisa mengi duniani kwani lina tamaduni zake binafsi.

Kwanza kanisa hili hukuwa na milango miwili kwa upande wa kulia na wa kushoto.

Wanaume hutumia mlango wa kulia wanapoingia kanisani, huku wanawake wakiingia kupitia mlango wa kushoto. Mpangilio huu hubaki vile vile huku wanawake wakikaa upande wa kulia  na wanaume wakiketi upande wa kushoto.

Kanisa hili huuthuriwa Siku ya jumamosi kinyume na Siku ya jumapili.

La kushangaza ni kuwa kanisa hili lina wafuasi wengi zaidi ikilinganishwa na makanisa mengine ambayo husemekana kuwa za kawaida. Inasemekana zaidi ya watu elfu kumi na tano huuthuria  ibada ya kanisa hili.

Kanisa hili lina matawi kumi na maanne, kumi na tatu yakiwa nchini na moja ikiwa nchini Uganda.

Roho safi pia inapinga swala la ukeketaji wa wasichana ama wanawake huku wakisema si Sera takatifu kulingana na waanzilishi wa kanisa hili.

JERU

Rostin alisema kuwa sababu kubwa hasa ya kanisa hili kuwa na milango miwili ni kwa sababu alionyeshwa na roho mtakatifu kwamba wanaume wanastahili kukaa upande wa kulia na wanawake  upande wa kushoto.

Kanisa hili pia hukuwa na Bendera ambayo Imechorwa alama tatu .moja ikiwa ni msalaba iliosimamishwaa ,nyingine ni msalaba iloliolazwa na hatimaye alama ya nyuni yaani aina ya ndege.

Mkuu huyo alieleza kuwa ndege inaamaanisha roho mtakatifu, msalaba iliosimamiswa inamaanisha uwepo wa Yesu kristu huku msalaba iliolazwa ikimaanisha hakutakuwa na  mateso tena duniani kwa wana wa Mungu.

UCHAGUZI 2017

BY PATRICK LEPAKIO

Huku uchaguzi mkuu wa agosti nane ukiendelea kukaribia serikali imekuja na mikakati ya kuhakikisha kwamba kampeni zitafanyika kwa njia ifaayo.

Joto la kisiasa limeendelea kuongezeka nchini, kufuatia uchaguzi wa agosti nane ambayo umeonekana kukaribia kila kukicha.

OCPD wa mji ongata rongai Silas ringera, ameeleza kuwa serikali iko tayari kuhakikisha kwamba wanasiasa watafanya kampeni zao kwa njia ambazo hazitasababisha vurugu nchini.

RONGAI

Ringera amesema kuwa baadhi ya mikakati ya kuhakikisha kuwa kampeni zitafanyika kwa amani billa rabsha ni kutuma walinda usalama wahuthurie mikutano za kisiasa na kuhakikisha kwamba imeendeshwa vilivyo.

Afisa huyo aliongeza kuwa yeyote atakaye patikana na makosa ya kuwachochea wananchi atachukuliwa hatua za kisheria na kutahatharisha vijana kutumiwa na wanasiasa kusababisha vurugu humu nchini haswa wakati wa kisiasa huku akisema watachukuliwa pia hatua za kisheria iwapo watajitosa katika uhalifu huo.

Ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa elfu mbili na saba na nane mtawalia ndiyo chanzo hasa iliyopelekea  Serikali kufatufa mbinu na mikakati ya kuhakikisha kuwa ghasia kama hizo hizatashuhudiwa tena nchini.